Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Timu ya Taifa ya Ngumi, Said Omary Gogopoa amesema, wadau mbalimbali wanatakiwa kujitokeza ili kufanikisha timu hiyo kuweza kushiriki mashindano mbalimbali kwa ajili ya majaribio ambayo itawasaidia kuweza kujiweka tayari kwa ajili ya mashindano hayo na kuweza kutimiza ahadi ya ushindi kwa watanzania.
Gogopoa amesema, mapambano ya majaribio yatasaidia kuweza kuona uwezo wa bondia mmoja mmoja ambao utasaidia kuweza kutambua sehemu ya kufanyia marekebisho ili kuweza kuwafanya mabondia hao kufanya vizuri katika mashindano hayo na mengine yaliyo mbele yao.