
Bondia bingwa wa WBF Thomas Mashali simba asiyefugika ama rais wa getho yuko katika maandalizi makali yakujiwinda na mpambano wake wa ubingwa wa dunia WBU universal atakapopambana na bondia Japhet Kaseba mwishoni mwa mwezi huu
Mashali amesema kuwa anafahamu uwezo wa mpinzania wake na ndio maana anajifua zaidi hasa kwa kucheza mapambano ya mazoezi na mabondia tofauti tofauti katika gym ili kujiweka fiti zaidi kitu ambacho kitamrahisishia kuibuka na ushindi mkubwa