Alhamisi , 17th Dec , 2015

licha ya kuendelea vyema na mazoezi ya maandalizi kushiriki mashindano ya kufuzu kucheza Olimpiki mwakani yatakayofanyika huko Casablanca Timu ya Taifa ya ngumi inakabiliwa na shida ya sehemu ya kufanyia mazoezi hayo.

Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga akiwa Makao Makuu ya Chama cha Ngumi,Uwanja wa Taifa .

Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi nchini Tanzania BFT Makore Mashaga ameiambia East Africa Radio kuwa kumekuwa na urasimu wa matumizi ya uwanja wa ndani wa Taifa ambao upo maalumu kwa matumizi ya michezo mingine kama ngumi na kikapu.

Mashaga ameitaka Serikali na wadau kusaidia kutatua changamoto za kukosekana kwa vifaaa na maeneo ya kufanyia mazoezi jambo ambalo limekuwa sugu kwa Tanzania haswa kwa michezo iliyopo nje ya soka.

Ameongeza kuwa anashangazwa na kukosa nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa ndani Taifa jambo ambalo anaamini ni kinyume na utaratibu huku ikionekana wamiliki wakiendesha programu nyingine ambazo zinawalazimu kushindwa kufanya maandalizi.

Hata hivyo Mashaga amesema anaimani na uongozi mpya wa wizara husika utaingilia kati na kubaini watu wanaohujumu michezo kwa kutumia mamlaka waliyonayo kutumia maeneo hayo kwa manufaa yao binafsi.