Ijumaa , 8th Apr , 2022

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa kibali kwa klabu ya Simba kuingiza mashabiki 60,000 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali dhidi ya klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaochezwa jumapili ,Aprili 17, 2022 .

(Mashabiki wa Simba wakiwa wameujaza uwanja wa Benjamin Mkapa)

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa klabu ya Simba kuruhusiwa kuingiza idadi kubwa ya mashabiki uwanjani na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) tangu kuzuka kwa maambukizi ya virusi vya uviko 19 huku mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa ,jijini Dar es Salaam.

Kuelekaa mchezo huo tayari klabu ya Simba imeanza kuuza tiketi ambapo kiingilio cha chini ni shilling elfu 3000 huku daraja la VIP A likiwa ni shilling elfu 30,000 huku mchezo huo ukitumia teknolojia ya VAR kwa mara ya kwanza hapa nyumbani Tanzania