Ijumaa , 13th Oct , 2023

Mlinda mlango namba moja wa Simba SC Aishi Manula amerejea kwenye mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje ya uwanja toka mwezi April na baadae mwezi June alifanyiwa upasuaji wa nyama za paja.

Manula ameonekana kwenye picha ya pamoja akiwa anafanya mazoezi pamoja na magolikipa wengine wa Simba SC Ahmed Feruzi, Abel Hussein, Ally Salim na Ayoub Lakred ikiwa ni kwa mara ya kwanza akionekana akifanya mazoezi ya pamoja, siku za nyuma alikuwa akifanya mazoezi binafsi yap eke yake.

Simba imerejea mazoezini jana Alhamisi Oktoba 12,2023 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi hicho kuelekea kwenye mchezo wa African Football League dhidi ya AL Ahly mchezo utakaochezwa Oktoba 20, 2023.