Jumatano , 22nd Jun , 2022

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane amekamilisha usajili wa kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani akitokea Liverpool ya England kwa ada ya uhamisho ya pauni million 35 ambayo ni zaidi ya Billion 99 (kwa pesa ya Tanzania.

Sadio Mane amesaini miaka 3 Bayern Munich

Mane mwenye umri wa miaka 30 amesaini mkataba wa miaka 3 na Bayern Munich, na anaondoka Liverpool baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 6, alijiunga na timu hiyo kutoka mitaa ya Merseyside mwaka 2016 akitokea Southampton.

Ameichezea Liverpool jumla ya michezo 269 na amefunga mabao 120 ameshinda makombe 6 ikiwemo Ubingwa wa Ligi Kuu England EPL na Ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA Champions League.

Na msimu uliopita wa 2021-22 Mane alifunga mabao 23 kwenye michezo 51 kwenye mashindano yote akiisaidia Liverpool kushinda makombe mawaili, Carabao Cup na FA Cup lakini pia Liverpool ilicheza fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya wakafungwa na Real Madrid na walimaliza nafasi ya pili kwenye EPL nyuma ya mabingwa Manchester City.