Mahakama moja ya Brazil imezuia mali za mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar kwa makosa ya kutokulipa kodi.
Mahakama hiyo iliyopo Sao Paulo ilitangaza kuwa inatoa waranti ya kuzuia mali yenye thamani ya takriban dola milioni 50 ya mchezaji huyo wa Brazil,ambapo imezuia ndege,jahazi la kifahari na Mali nyengine.
Neymar mwenye umri wa miaka 23 ametuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa namshataka ya kujibu, ingawa mwenyewe amekana kufanya makosa yoyote.
Miongoni mwa mali zilizozuiwa ni kampuni tatu zinazomilikiwa na familia yake.
Waendesha mashtaka wanamtuhumu Neymar kwa kuanzisha kampuni ambazo zilimsaidia kulipa kiwango kidogo cha ushuru.
Wanataka alipe dola milioni 16 kama kodi ambayo haikutangazwa.
Hatahivyo Neymar anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama na kwamba sio rahisi kwa yeye kuhudumia kifungo, kulingana na mkaguzi mmoja wa maswala ya fedha.






