Baadhi ya wanamichezo wa kuogelea wakichuana katika michuano iliyopita ya taifa.
Kozi ya makocha wa mchezo wa kuogelea nchini imeendelea hii leo jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa leo ni siku ya sita ambapo kozi hiyo hii leo imeingia katika progaram ya mazoezi ya vitendo kwa walimu na makocha wa kuogelea kufanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo
Mkurugenzi wa ufundi wa chama cha kuogelea nchini Tanzania TSA Marcelino Ngalioma amesema kozi hiyo ni moja ya mipango ya muda mrefu ya chama hicho katika kuhakikisha mchezo huo unakua hapa nchini na chama kimejipanga kuhakikisha kunakuwepo na kozi za mara kwa mara za ndani na nje ya nchi kwa makocha ili baadae waje wawafundishe walimu wengine na kupelekea kukua kwa mchezo huo kote nchini.
Kozi hiyo inaendeshwa na mkufunzi kutoka chama cha kuogelea duniani FINA Matthias Ludwing ambaye amestaajabu kwa uwezo wa makocha wa hapa nchini kitu ambacho hakutegemea kukiona kwa level yetu
Aidha mkufunzi huyo Ludwing amesema makocha wengi wa Tanzania hasa waliohudhuria kozi hiyo ni makocha wenye uzoefu mkubwa kitu ambacho kinamrahisishia utendaji wake wa kazi na anatoa shukrani kwa chama cha kuogelea nchini Tanzania TSA kwa kumpa ushirikiano wa kutosha tangu ilipoanza kozi hiyo Juni 20 mwaka huu na anamatumani makubwa kozi hiyo itakuwa njia ya kuelekea kwenye mafanikio ya mchezo wa kuogelea.