
Mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad Kawemba amesema, St George imetuma barua rasmi ya kumwalika Friday akafanye majaribio ya wiki moja, ambayo akifuzu atasajiliwa lakini wao kama uongozi bado wanaifanyia kazi barua hiyo waliyoipokea jana asubuhi na watajua anatakiwa kwenda huko lini baada ya kuwasiliana nao.
Friday ni mmoja ya wachezaji waliokulia Academy ya Azam FC na kupandishwa timu kubwa, huku akiwa na uwezo wa kupiga mashuti ya mbali ambapo St George hivi sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mholanzi Mart Nooij, ambaye amewahi kumuita mara kwa mara Friday kwenye kikosi cha Stars akianzia na Taifa Stars Maboresho.