Ijumaa , 7th Nov , 2014

Mechi za Ligi kuu Tanzania Bara, Msimu wa kwanza mzunguko wa saba zinaendelea kesho kwa mechi Nne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Yanga SC itaikaribisha Mgambo ya jijini Tanga huku mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam FC wakiwakaribisha wagosi wa kaya Coastal Union kutoka jijini Tanga mechi itakayopigwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Katika mechi nyingine, Stand United itashuka dimbani kuikaribisha Mbeya City Uwanja ya Kambarage mjini Shinyanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mwenyeji wa Kagera Sugar mechi itakayochezwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.