
Bao la Paul Nonga dakika ya 38 limeipa Mwadui FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Toto ambapo ushindi huo unakuwa ushindi wa pili kwa Mwadui katika michuano hiyo inayoandaliwa na Chama cha Soka Shinyanga (SHIREFA).
Katika michezo ya awali, Mwadui iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu huu pamoja na Toto Africans iliifunga mabao 4-0 Stand United ambapo Toto ilishinda 1-0 katika mchezo wake wa kwanza hapo juzi dhidi ya Kagera Sugar.
Michuano hiyo inaendelea leo hii kwa kupigwa mchezo kati ya Kagera Sugar na Stand United.