
Mechi nyingine itakuwa kati ya Mbeya City, ambayo itakuwa mgeni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Ambapo kocha msaidizi wa Mbeya City Maki Mwalwisi amesema kuwa mchezo dhidi ya Ashanti United inayofundishwa na Abdallah Kibaden utakua mgumu kutokana na Ashanti ipo katika mkakati wa kukwepa kushuka daraja lakini wao wamekuja kupambana na timu iko vizuri kwaajili ya kuibuka na ushindio hapo kesho.