Jumatatu , 3rd Nov , 2014

Michuano ya Ligi Daraja la pili Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Novemba 22 mwaka huu katika viwanja mbalimbali nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema kamati ya mashindano ikiwa chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Geofrey Nyange Kaburu ilikaa na kupitia maandalizi ya ligi hiyo na kutoa mwongozo wa Ligi hiyo.

Wambura amesema wameongeza muda wa usajili kwa timu shiriki za Ligi hiyo kutokana na Timu takribani Nne kushindwa kuwasilisha usajili wao kwa muda uliopangwa.