Jumapili , 10th Jun , 2018

Klabu ya Leicester City kutoka nchini England, imeonesha nia ya kumtaka kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ili kumrithi kocha wa sasa Claude Puel katika msimu ujao wa Ligi kuu England 2018/2019.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun limeripoti leo Juni 10, 2018 kwamba kocha Brendan Rodgers, ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Celtic kutoka nchini Scotland anapewa nafasi kubwa baada ya kuonesha mafanikio kwa kuipatia mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Scotland katika kipindi cha miaka miwili tangu ajiunge na klabu hiyo.

Kocha wa sasa Claude Puel, huenda akaondoka kabla ya kuanza msimu ujao wa ligi na hivyo nafasi yake ikachukuliwa na Brendan Rodgers.

Uongozi wa Leicester City, awali ulionekana kumtaka kocha wa zamani wa Arsenal , Arsene Wenger na kocha wa Newcastle United, Rafael Benitez,  lakini Brendan Rodgers ndiye anaepewa kipaumbele zaidi na mabingwa hao wa England mwaka 2016.

Malengo makubwa ya Leicester City, ni kumaliza katika moja ya nafasi sita za juu katika Ligi Kuu ya England kwa msimu ujao ili kuweza kushiriki michuano ya Ulaya.