
Ndoto za lakers zilizimwa na timu ya Phoenix Suns na kuondoa matumaini ya
LeBron James kutwaa ubingwa wake wa tano msimu huu baada ya kuichapa Lakers kwa alama 121-110 katika dimba la Footprint Center.Lakers ipo mbioni kuachana na kocha wake Frank Vogel msimu huu utakapo malizika kutokana na mwenendo mbovu licha ya kuwa na staa aliyewahi kushinda tuzo ya MVP kama Russell Westbrook na wachezaji mahiri kama Anthony Davis.