
Wakati timu 50 za Wanawake na Wanaume za mpira wa wavu wa ufukweni zikiendelea kuoneshana kazi jijini Dar es Salaam chama cha mchezo huo jijini humo kimesema matunda ya kuendesha kozi kwa makocha na waamuzi yameanza kuonekana.
Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam DAREVA Siraju Mwasha amesema kuwa mara kadhaa kumekuwa na malalamiko juu ya maamuzi lakini kwa sasa kila kitu kinaenda sawa na wanataraji ligi yao kumalizika mwezi Novemba mwaka huu.
Mwasha amesema mchezo wa mpira wa wavu unaochezwa viwanja vya ndani ni tofauti na wavu ya ufukweni, hivo kitendo cha kutoa mafunzo kwa walimu na waamuzi wa mchezo huo kabla ya kuanza kwa ligi, kumeleta mabadiliko ambayo hivi sasa mashindano yanenda vizuri kwa kuwa yameboreshwa.
Mechi za mchezo huo zitaendelea kesho katika viwanja vya Mbalamwezi badala ya viwanja vilivyokuwa vikitumika hapo awali.