Jumatatu , 10th Aug , 2015

Chama cha Mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA kimesema kinatarajia kutoa kozi kwa waamuzi wa mchezo wa wavu wa Ufukweni na Uwanjani ili kuwa na waamuzi wengi watakaoweza kuchezesha mashindano ya Klabu Bingwa Taifa.

Akizungumza na East Africa Radio, mjumbe wa kamati ya maandalizi na ufundi ya Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Nassoro Shariff amesema, kozi hiyo inatarajia kuanza Septemba saba mpaka 13 mwaka huu kwa kushirikisha waamuzi 35 kutoka jijini Dar es salaam.

Sharif amesema, kozi hiyo itasaidia kutoa waamuzi watakaoweza kuchezasha mchezo wa mpira wa wavu wa ufukweni unaotarajiwa kuanza Septemba 26 mpaka Novemba 29 mwaka huu.