
Hayo yameelezwa na mwanasheria Bashir Yakub kupitia MJADALA wa East Africa Television unaoruka kila siku kuanzia saa 1:30 usiku, ambapo amebainisha kuwa mtuhumiwa wa makosa ya mtandaoni yupo hatarini muda wote.
''Unajua makosa ya mtandao yana tofauti kubwa na makosa mengine, mtu anaweza kukamatwa na kushtakiwa hata baada ya miaka 20 kupita tangu atende kosa hilo'' , amesema Mwanasheria huyo.
Aidha Bashir ameongeza kuwa mtu hawezi kuomba radhi na kusamehewa kwa kutenda kosa la kimtandao kwani sheria haimpi mtu nafasi hiyo.
''Unaweza ukaona makosa ya kimtandao yanafanywa na watu maarufu lakini wakienda TCRA wanaomba msamaha na wanaachwa wakati sheria haina kipengele hicho, hivyo sheria hii ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015, haijasimamiwa vizuri na mamlaka husika'', ameongeza.