Ijumaa , 5th Jun , 2015

Mashindano ya mpira wa kikapu ya kombe la Muungano yaliyokuwa yakitarajiwa kufanyika Juni 20 mpaka 28 yamesogezwa mbele ambapo yatafanyika Julai 22 mwaka huu ili kupisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Akizungumza na East africa Radio, kamishna wa ufundi na mipango wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF, Manase Zablon amesema, anaamini kwa muda walioupanga washiriki wa michuano nhiyo watakuwa huru kwa ajili ya ushiriki.

Manase amesema, timu shiriki za mashindano hayo ni timu nne zilizoingia nusu fainali katika ligi kuu ya Taifa NBL na ile ya Zanzibar huku kwa wanawake zikishiriki timu zote kutokana na timu hizo kuwa chache.

Manase amesema, kwa muda uliotolewa anaamini vilabu shiriki vitaendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ili kuweza kuleta changamoto za kiushindani katika michuano hiyo.