Jumapili , 8th Oct , 2023

Wapinzani wa Yanga SC hatua ya makundi ya CAFCL, CR Belouizdad ya Algeria imemfuta kazi kocha wa zamani wa Simba SC, Sven Vandenbroeck kama kocha mkuu klabuni hapo kwa makubaliano ya pande zote kutokana na kutofautiana kimtazamo.

Taarifa klabu hiyo leo Oktoba 8, 28023 imebainisha kuwa:- “Mwenyekiti wa Bodi ya vijana ya CR Belouizdad, Bw. Mahdi Rabhi, amesitisha mkataba wa kocha wa Ubelgiji "Svan Vandenbroek" kwa makubaliano ya pande zote na kumuondoa kwenye benchi la ufundi la timu kutokana na utofauti wa kimtazamo kati ya pande zote.”

CR Belouizdad jana ikiwa nyumbani ilikumbana na kipigo cha 3-2 dhidi ya USM Khenchela kwenye mchezo wa Ligi Kuu Algeria ikiwa nafasi ya 11 kwenye mchezo wa Ligi hiyo alama 3 baada ya mechi mbili.

CR Belouizdad imepangwa kundi D kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na Al Ahly ya Misri, Yanga SC ya Tanzania na Medeama ya Ghana.