Alhamisi , 27th Nov , 2014

Kocha wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Patrick Phiri anatarajia kuanza mazoezi rasmi kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya nani mtani Jembe inayotarajiwa kufanyika Desemba 13 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Suleiman Matola amesema timu hiyo inaendelea na mazoezi ambapo anaendelea kuisimamia tangu kocha alipokuwa likizo.

Matola amesema baadhi ya wachezaji katika kikosi hicho hawajawasili na bado hawajapata taarifa zao lakini bado wanafuatilia ili kuweza kujua tatizo lililopelekea hadi wachezaji hao hawajawasili mazoezini.