Kocha mpya wa klabu ya Simba, Joseph Omog kushoto akikabidhiwa jezi na Rais wa klabu hiyo Evans Aveva, wakati aliposaini kuifundisha klabu hiyo kwa mkataba wa miaka 2, Julai 1, 2016
Uongozi wa klabu ya Simba umetetea tabia yao ya kuwaangalia makocha wapya wa klabu hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja, hata kama kocha hajazoeana na aina ya wachezaji aliowakuta.
Mwenyekitia wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zakari Hans Poppe amesema kocha mpya wa klabu hiyo Mcameroon, Joseph Marius Omog atatumia wachezaji aliowakuta na wengine atakaowasajili yeye, ili kutengeneza kikosi cha mafanikio kwa msimu ujao wa ligi.
Poppe amesema, kocha yeyote anayejua, huwa anatumia hata wachezaji aliowakuta na timu inaweza kufanya vizuri.
Hadi sasa Simba imeongeza wachezaji 11 chini ya kamati ya usajili ya klabu hiyo, wengine wakiwa wameshasajiliwa na wengine wakiwa kwenye majaribio.
Wachezaji 11 wapya waliopo kambi ya Simba mkoani Morogoro ni, Mohammed Kijiko, Moses Chibandu, Said Mussa, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Frederick Blagnon, Kelvin Falu, Vincent Costa, Method Mwanjali, Janvier Besala Bokungu na Mussa Ndusha.



