Jumatatu , 18th Jul , 2022

Klabu ya Polisi Tanzania imefikia makubaliano ya kutoendelea na aliyekuwa kocha wake Malale Hamsini katika msimu ujao wa 2022/2023.

Kocha Malale Hamsini

Maamuzi hayo ni baada ya makubaliano ya pande zote mbili kwa maana ya uongozi wa Polisi na kocha Malale.

Malae alijiunga na Polisi Tanzania mwaka 2019 akichukua mikoba ya Selemani Matola aliyetimkia Simba kipindi hicho na ameiongoza timu hiyo kwa misimu mitatu.

Msimu uliopita Malale aliingoza Polisi kumaliza nafasi ya nane ikicheza mechi 30, kushinda nane sare 13 na kupoteza tisa na kuvuna alama 37.

Taarifa ilizonazo Mwanaspoti, kocha huyo huenda akajiunga na Mbeya City muda wowote kuanzia sasa.

Mecky Mexime anayeinoa akademi ya Cambiasso, Salum Mayanga wa Mtibwa Sugar na Mathias Lule wa Mbeya City ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuhitajika kumrithi Malale Polisi.