
Kilimanjaro Stars imeondoka kwenye michuano hiyo na alama moja pekee iliyoipata kwenye sare dhidi ya Libya. Mapema leo Zanzibar Heroes ilicheza na Libya na kupoteza 1-0 lakini tayari imeshakata tiketi ya nusu fainali.
Zanzibar Heroes itacheza na mabingwa watetezi Uganda Disemba 15, katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya, Disemba 15, mwaka huu.
Nusu Fainali ya kwanza itawakutanisha wenyeji Kenya dhidi ya Burundi Desemba 14. Mchezo wa Kilimanjaro Stars na Kenya umechezwa kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta, Kenya.