Jumatano , 27th Mei , 2015

Michuano ya ligi ya mpira wa kikapu ya majiji Afrika Mashariki na kati yameanza leo uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha timu kutoka majiji 10 ya Afrika mashariki na kati.

Akizungumza na East Africa Radio, mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Tanzania TBF, Manase Zabroni amesema timu hizo zimegawanyika ambapo timu saba ni za wanaume na timu tatu za wanawake.

Zabroni amesema, majiji hayo ni Mogadishu, Qardo, Dar City, Dar dream Team, Tanga na Mbeya, Nairobi, Kampala, na Egypy.

Zabroni amesema, michuano hiyo inalenga kuweka umoja katika majiji ya Afrika Mashariki na kati ambayo yapo katika kanda ya tano na hapo baadaye kuweka katika mtaala wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani FIBA ili kuweza kuwa na mashindano makubwa zaidi ya hayo.