Jumatano , 3rd Dec , 2014

Chama cha Mpira wa kikapu nchini TBF kimesema hivi sasa wapo katika mpango wa kuandaa timu ya Taifa ya mchezo huo ili kuweza kuuboresha mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa TBF, Saleh Zonga amesema michuano ya Klabu bingwa Taifa iliyomalizika imesaidia kuweza kujua vipaji vya wachezaji kutoka katika vilabu mbalimbali nchini hivyo itakuwa rahisi kuweza kupata timu nzuri ya Taifa itakayoweza kushiriki mashindano mbalimbali makubwa kwa ndani na nje ya nchi.

Zonga amesema vilabu shiriki vya michuano mbalimbali hapa nchini vinatakiwa kuanza maandalizi mapema ya michuano mbalimbali ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo.