Mashabiki wa mchezo wa riadha nchini Kenya wakionyesha mabango ya kupinga urasimu kwenye mchezo huo nchini mwao.
Taarifa zilizopo ni kwamba Kenya haikuweza kutoa uthibitisho kwa shirika la kukabiliana na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli duniani WADA na kwamba huenda ikaorodheshwa miongoni mwa mataifa yaliyopo katika hatari ya kukiuka sheria ya shirika hilo.
Taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo wanariadha wake wametawala katika mbio ndefu duniani, litapewa miezi miwili kuanzisha sheria na ufadhili la sivyo liorodheshwe kuwa miongoni mwa mataifa ambayo hayajatimiza matakwa ya WADA.
Hii itamaanisha kwamba huenda Kenya ikapigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya Olimpiki, ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil, pamoja na michezo mingine mkubwa.





