Jumapili , 17th Dec , 2017

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imelipa kisasi dhidi ya timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa kuifunga katika mchezo wa fainali ya CECAFA Senior Challenge uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kenyatta Machakos Kenya.

Mchezo huo wa fainali ulikuwa na kila aina ya mvuto baada ya Kenya kutangulia kwa bao la mapema dakika ya tano, bao ambalo lilidumu kwa zaidi ya dakika 80 ambapo Zanzibar Heroes ilisawazisha dakika ya 87.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1, mwamuzi aliongeza dakika 30 ambapo Kenya walifunga bao la pili dakika ya 97.

Zanzibar hawakupotea mchezoni ambapo walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 99 na kufanya dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Fainali ya leo ni fainali ya 39 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo ikiwa ni ubingwa wa saba kwa taifa la Kenya. Fainali hiyo pia ilikuwa ni kumbukumbu ya fainali ya 1995 ambapo Zanzibar iliifunga Kenya mabao 2-1 na kutwaa ubingwa hivyo leo Kenya imelipa kisasi.