Alhamisi , 7th Apr , 2022

Mabingwa wa tetezi wa Ligii Tanzania bara Simba SC imepunguza tufauti ya alama kati yake na vinara wa ligi Yanga kutoka alama 14 mpaka 11 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, jioni ya leo Aprili 7, 2022 mchezo uliochezwa Mkwakwani Tanga.

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere (kulia) akishangilia baada ya kufunga bao la pili lililowapa ushindi Simba

Simba walingia kwenye mchezo huu wakiwa wamezidiwa alama 14 na watani zao Yanga ambao ndio vinara wakiwa na alama 51 ambazo wamezifikia baada ya kushindi dhidi ya Azam FC hapo jana kwa mabao 2-1. Hivyo wekundu wa Msimbazi walihitaji ushindi kwenye mchezo huu ilikupunguza tofauti hiyo ya alama ilikuweka matumaini katika mbio za ubingwa.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Bernald Morrison dakika 40, na kiungo Victor Patrick Akpan akaisawazishia Coastal dakika ya 78 na Meddie Kagere kuifungia Simba bao la pili na la ushindi dakika ya 90.

Kwa ushindi huu Simba imefikisha alama 40 ikiwa ni tofauti ya alama 11 dhidi ya Yanga vinara wa Ligi wenye alama 51 katika michezo 19 na wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Simba wenye michezo 18. Mchezo unaofata wekundu wa Msimbazi wanacheza dhidi ya Polisi Tanzania Aprili 10 2022. Uwanja wa Ushirika Moshi.