
Jonesia Rukyaa
Rukya amejumuishwa katika orodha ya waamuzi hao kama mwamuzi wa kati akiwa ni mtanzania pekee katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 17 hadi Desemba 1, 2018.
Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza jumla ya waamuzi wa kati 13 na waamuzi wasaidizi 12 ambao watakuwa jijini Acra Ghana kwaajili ya kuhakikisha mechi zote zinakwenda sawa mpaka fainali.
Fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazowakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake zitakazofanyika mwakani nchini Ufaransa.
Timu tatu zitakazo maliza katika nafasi za juu kwa maana ya bingwa, mshindi wa pili na mshindi wa tatu watafuzu kucheza Kombe la Dunia la wanawake.