Jumapili , 14th Dec , 2014

Wananchi wametakiwa kujitokeza ili kusaidia kukuza michezo kwa vijana hap nchini ili kupata vipaji vipya na timu nzuri ya taifa ya vijana.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kituo cha kukuza vipaji vya vijana, Iddy Kipingu amesema Serikali peke yake haitoshi kusaidia kukuza vipaji hivyo, hivyo wananchi pia wana mchango mkuwa katika kukuza michezo nchini.

Kipingu amesema iwapo jamii itajitokeza kwa ajili ya kusaidia vijana wanaamini timu hizi zina uwezo wa kufika mbali na kulitangaza Taifa katika michezo.