Alhamisi , 14th Jul , 2016

Meneja mpya wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anapanga kutosafiri na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic kwenda china.

Zlatan Ibrahimovic

Mourinho hata hivyo amepanga kuwachukua wachezaji wa England Wayne Rooney, Chris Smalling na Marcus Rashford.

Klabu hiyo inapanga kucheza mechi mbili za kujiandaa kwa msimu ujao na imepangiwa kuwasili Uchina Jumanne.

Hata hivyo Mourinho amesema Rooney, Smalling na Rashford hawatacheza dhidi ya Borussia Dortmund mjini Shanghai tarehe 22 Julai na Manchester City mjini Beijing mnamo 25 Julai.

Alisistiza kuwa Ibrahimovic, 34, huenda asishirikishwe hata kidogo.

Akikosa kusafiri na timu hiyo bara Asia, basi mashabiki watasubiri muda zaidi kumtazama Ibrahimovic akicheza mechi yake ya kwanza United.

United wanatarajiwa kucheza dhidi ya Salford City uwanjani Moor Lane mnamo 26 Julai.

United baadaye watacheza dhidi ya Galatasaray mjini Gothenburg nchini Sweden, nchi anamotoka Ibrahimovic tarehe 30 Julai.

Kisha, watakutana na Everton mechi ya heshima kwa Wayne Rooney Old Trafford mnamo 3 Agosti kabla ya kukutana na mabingwa wa Ligi ya Premia kwa mechi ya Community Shield mnamo 7 Agosti.