
Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim Twaha “Messi”
Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao ambapo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Kwa upande wake,Ibrahim Twaha “Messi” amesema, amerudi nyumbani kwa mara nyingine na anaahidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.