Jumatano , 28th Sep , 2016

Timu ya Mbao FC imeahidi kuchukua pointi tatu mbele ya Ndanda FC hii leo katika mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara utakaopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kikosi cha Mbao FC

Msemaji wa Mbao, Crisant Malinzi amesema wamejiandaa vizuri na hawawezi kuiogopa Ndanda kutokana na matokeo waliyoyapata dhidi ya Azam FC.

“Tumejiandaa vizuri na tutafanya vizuri na kushinda kwani vijana wako tayari na hatuna hofu na suala la wao kuwafunga Azam FC,” amesema Malinzi.

Mbao FC ndiyo imepanda daraja msimu huu lakini bado haijawa na mwenendo mzuri.