Ijumaa , 11th Dec , 2015

Vinara wa Ligi kuu Tanzania Bara Azam Fc wamesema, hawajajiandaa na mchezo dhidi ya Simba Sc pekee hapo kesho kwani watacheza na utakwisha hivyo maandalizi yao ni kwa mechi zote za Ligi zilizobakia.

Afisa Habari wa Azam Fc Jaffary Iddy Maganga amesema, Kocha Stewart Hall amekiandaa kikosi chake kwa ajili ya kuweza kuibuka na Pointi tatu muhimu.

Maganga amesema, wanaamini wataibuka na Pointi tatu kwani kikosi kipo vizuri hata kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kutokana na usajili wao pamoja na ubora wa Benchi la Ufundi hivyo wanaamini watadhihirisha ubora wa Timu yao hapo kesho kwa kucheza na kupambana kwa kutafuta Pointi tatu na kuendelea kujiweka kileleni mwa Ligi kuu.