Alhamisi , 19th Jun , 2014

Kamati ya rufaa ya shirikisho la soka nchini TFF inakutana hii leo kwa kikao cha dharura kwaajili ya kusikiliza rufaa nyingine ya aliyekua mgombea wa nafasi ya urasi wa klabu ya Simba Michael Wambura ambaye ameondolewa na kamati ya uchaguzi ya Simba

Michael Wambura akiingia katika gari mara baada ya kuwasilisha rufaa yaek TFF.

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema bado linaendelea na mazungumzo na uongozi na kamati ya utendaji ya Simba kuhusiana na muhstakabali wa uchaguzi wa klabu hiyo uchaguzi ambao utakaofanyika june 29 mwaka huu

Rais wa TFF Jamal Malinzi awali amempongeza mwenyekiti wa klabu ya Simba na kamati yake ya utendaji kwa kutaka busara itumike ili kukamilisha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo ambao hivi sasa uko shakani kutokana na mapingamizi yanayoendelea kwa baadhi ya wagombea huku baadhi ya wanachama wakitishia kwenda mahakamani kusitisha uchaguzi huo.

Aidha Malinzi amesema kwakuliona hilo aliiagiza kamati ya rufaa kuketi hii leo ili kusikiliza rufaa nyingine iliyokatwa na Michael Wambura ambaye juzi alienguliwa kuwania nafasi ya kuwania urais wa klabu ya Simba kwa kile kinachodaiwa na kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo kuwa mgombea huyo amekiuka kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya wakati

Akimalizia Malinzi amesema lengo la kuchuakua uamuzi huo si kutaka kumbeba mgombea flani bali ni kuhakikisha busara inatumika na kuifanya klabu ya Simba imalize suala la uchaguzi salama na kuendelea na masuala ya kujenga timu hiyo.