Bingwa wa dunia mchezo wa magari ya langa langa, Lewis Hamilton ametwaa taji la 4 la British Grand Prix, baada ya kumaliza kinara hapo jana huko, Silverstone.
Ushindi huo unamfanya Hamilton, abakishe pointi 1 kumfikia dereva mwenza Mercedes, Nico Rosberg katika kinyanganyiro cha kuwania ubingwa wa dunia.
" Sijui kama unaweza kuwa na furaha kama niliyo nayo mimi".Alisema Hamilton, baada ya mbio hizo.



