Alhamisi , 9th Mar , 2017

Beki wa katikati tegemeo wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali ataendelea kuwa nje ya dimba kwa mwezi mzima wa Machi kutokana na maumivu ya goti.

Method Mwanjali, siku aliyopata majeraha

Mwanjali hajajumuishwa kwenye kikosi cha Simba kilichoondoka leo kwenda ziara ya Dodoma kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Polisi Jumamosi hii katika Uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kwamba Mwanjali hatakwenda Dodoma na hatahusishwa kwenye programu yoyote ya timu mwezi huu wa Machi.