Jumamosi , 31st Oct , 2015

Vigogo wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, Yanga na Mtibwa Sugar leo zimeondoka na ushindi mnono katika michezo yao ya ligi kuu iliyopigwa katika viwanja tofauti.

Vigogo wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, Yanga na Mtibwa Sugar leo zimeondoka na ushindi mnono katika michezo yao ya ligi kuu iliyopigwa katika viwanja tofauti.

Simba ilikuwa katika dimba la Taifa Dar es salaam ambapo imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1, ambapo Ibrahim Hajib ameweza kurejesha kiwango chake cha ufungaji kwa kuipatia Simba mabao matatu kati ya Sita, huku mengine yakifungwa na nyota wa klabu hiyo kwa msimu huu, mganda Hamis Kiiza.

Majimaji imejipatia bao la kufuta machozi kupitia kwa Ditram Nchimbi.

Mkoani Tabora, Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mabao yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 23 na Deus Kaseke dakika ya 64.

Mtibwa Sugar imeichapa Mwadui FC mabao 4-1 katika uwanja wa Manungu Morogoro wakati Coastal Union ikitoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City Mkwakwani Tanga.

Michezo mingne ya ligi hiyo itaendelea kesho na kesho kutwa kama ifuatavyo.

African Sports VS JKT Ruvu Stars
Azam FC VS Toto Africa
Tanzania Prisons VS Ndanda FC
JKT Mgambo VS Stand United