Jumamosi , 6th Feb , 2016

Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi, ameshusha presha kwa kurejea kikosini baada ya kupona maumivu ya tumbo huku akiahidi kuwepo uwanjani katika mechi ya watani wao wa jadi Simba.

Mwingi hadi hivi sasa amekosa mechi dhidi ya Majimaji FC waliyoshinda mabao 5-0 na nyingine ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga waliyofungwa mabao 2-0, pia dhidi ya Prisons waliyotoka sare ya mabao 2-2.

Beki huyo tangu ametua Yanga msimu huu wa Ligi Kuu Bara amejihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, akifanikiwa kumtoa Oscar Joshua.

Mwinyi amesema kuwa amepona na ameanza mazoezi binafsi ya kujiweka fiti zaidi ili mechi dhidi ya Simba aweze kucheza.