Jumamosi , 2nd Apr , 2022

Anaeleza Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara kupitia Instagram yake baada ya kukutana na kocha wa Simba Pablo Franco Martin mapema leo hii.

Haji Manara kulia akiwa na kocha wa Simba Pablo Martin

"Maeneo ya Sea Cliff mchana huu, nilipokutana na kocha wa Simba Pablo akiwa na mkewe na mtoto wao mdogo, akaniita kunisalimia na tukaongea machache huku akitukakia kheri kwenye mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Azam na mimi nikijibaraguza kumtakia kheri kesho".

"Sikuwahi kukutana nae before kumbe zile swaga zake za uwanjani ni temple tu ya mechi very humble guy and gentleman.Nilipenda tulipoagana aliponiambia msalimie Professor Nabil".