Alhamisi , 29th Jul , 2021

Haji Manara aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano pale Msimbazi, amefanya kazi kubwa ya kuongeza thamani chapa ya klabu ya Simba na mchezo wenyewe wa soka nchini kutokana na namna yake ya utendaji kazi.

Picha ya Haji Manara

Mbinu zake za kucheza na saikolojia za watu zilizojazwa na propaganda ndani yake zilifanikiwa na vitabaki kwenye kumbukumbu ya wadau wengi wa soka ndani na nje ya Tanzania kwani yapo mengi ya msingi ya kuiga kutoka kwake.

Manara ameacha alama kubwa kwenye mioyo ya mashabiki wa pande zote kupitia;

1.Misemo (slogans) iliyokuwa inaibua ari ya upambanaji kwa wachezaji na hamasa kwa mashabiki kwenye michuano ya kimataifa ambayo ilikuwa ikichezwa uwanja wa nyumbani (Benjamin Mkapa Stadium) mpaka kujengeka kwa dhana ya yeyote atakaye kanyaga Taifa hatoki mfano War in Dar (Vita Ndani ya Dar).

Misemo hiyo wakati mwingine ilikuwa ikiwakera mpaka watani zao wa jadi Yanga.

2.Manara alijitahidi kutengeneza hamu,  kuongeza ladha na kuvutia wadau na wapenda soka kutamani mchezo huo kwa kuamsha hisia kabla na baada ya mchezo.

3.Pia ni moja ya wasemaji waliofanikiwa kuibua mijadala mingi kwenye vijiwe vya michezo, inawezekana kuto kuwepo kwake kwenye moja ya hivi vilabu vikubwa kunaweza kupunguza mijadala hiyo.