Ijumaa , 21st Jan , 2022

Algeria yavuliwa ubingwa wa michuano ya matiafa barani Afrika AFCON baada ya kufungwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi na wamemaliza wa mwisho kwenye kundi E wakiwa na Alama 1.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria

Ni kwa mara ya 5 kwenye fainali 6 za AFCON zilizopita bingwa mtetezi anatolewa hatua ya makundi na Algeria walihitaji ushindi kwenye mchezo dhidi ya Ivory ili kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano ya 16 bora, lakini wamepoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-1, mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Frank Kessy, Ibrahim Sangare na Nicolas Pepe waki lile la Algeria limefungwa na Sofiane Bendebka.

Kipigo hicho kimeifanya Algeria kuvuliwa ubingwa wa michuano ya AFCON baada ya kumaliza wa mwisho kwenye kundi E. Ivory Coast wamemaliza vinara wa kundi hilo wakiwa na alama 7, Equtoria Guinea wamemaliza nafasi ya pili wakiwa na alama 6 wakati Sierra Leone wameamaliza watatu na alama 2.

Algeria waliingia kwenye michuano hii wakiwa hawajafungwa kwenye michezo 35 mfululizo lakini walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Equtoria Guinea kwa kufungwa bao 1-0, kabla ya kufungwa na Ivory Coast na mchezo wa kwanza walitoka suluhu na Sierra Leone.

 

 

Baada ya michezo ya makundi kukamilika jana, hatua inayofata ni ya mtoano ya 16 bora na ratiba ni kama ifuatavyo.

Burkina Faso Vs Gabon

Nigeria Vs Gambia

Cameroon Vs Comoros

Senegal Vs Cape Verde

Morocco Vs Malawi

Ivory Coast Vs Misri

Mali Vs Equatorial Guninea