
Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Simba
Usajili unaotikisa hivi sasa nchini n wa klabu kubwa za Simba, Yanga na Azam FC, huku Simba wakifanya kwa staili tofauti ya kutambulisha mchezaji kila siku za kazi, majira ya saa 7:00 mchana.
Leo imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajib aliyekuwa akiwaniwa na TP Mazembe kutokea klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na kukifanya kikosi hicho kuwa cha moto kuelekea msimu ujao wa ligi.
Kutana na shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba, akitaja kikosi matata anachokiamini kuwa ni cha ushindi msimu ujao, msikilize hapa chini.