![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/10/19/Snapinsta.app_391441994_1119793602333825_422691103619996571_n_1080.jpg?itok=8kqqqR8B×tamp=1697726513)
Waziri Ndumbaro amesema hayo kuelekea mchezo wa ufunguzi baina ya Simba dhidi ya Al Ahly ambapo utachezwa Ijumaa ya Oktoba 22-2023 huku mpaka sasa Marais 54 kutoka kwenye mashirikisho ya soka barani Afrika wakiwa tayari wamewasili hapa nchini kushuhudia mchezo huo.
“Mechi sio ndogo, ukiangalia Simba ni timu ya saba inakutana na timu iliyokuwa ya kwanza katika msimamo wa Afrika. Hii mechi kwa wachezaji wa Simba Sc ni kipimo tosha kwa kuona ubora wao”amesema Ndumbaro
Lakini pia unaona jinsi gani mashindano haya yalivyombeba kila mtu kwa sababu msanii wa Tanzania Ally Kiba atakuwa sehemu ya kuwapa burudani ya muziki kwa wageni watakashuhudia mchezo huo," amesema Ndumbaro.
Aliongeza kuwa Tanzania imepata heshima nyingine kwa mchezo wa TP Mazembe dhidi ya Esperance itachezwa hapa nchini katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
.