Golikipa wa Uganda, Dennis Onyango
Onyango ambaye ni mwanandinga bora wa ndani wa Afrika ambaye anakipiga na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, amesema anahisi ni muda wa kuwaachia vijana waoneshe uwezo wao kwa Taifa.
Onyango aliiongoza Uganda The Cranes kufuzu michuano ya Mataifa Afrika mwaka huu, na pia ameiongoza katika michezo mitatu ya hatua ya makundi na kupoteza michezo mitatu huku ikiambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wake wa mwisho ilyocheza jana dhidi ya Mali.