Mkufunzi wa kozi ya makocha mpira wa wavu kwa mkoa wa Dar es salaam Fredy Mshangama amesema wanafunzi watakaopokea mafunzo kutoka kwa walimu watakaomaliza kozi mbalimbali wategemee mabadiliko makubwa kwani wamelenga kufika mbali zaidi kwa makocha na wanafunzi kwa kuwa na kozi nyingi na za kuwawezesha makocha kuwa na uelewa wa mchezo huo.
Mshangama amesema, kwa vyama vya mikoani vinatakiwa kusaidia vyama vya taifa kwa kuvishawishi kuweza kufikia mbali katika malengo waliyojiwekea ya kukuza mchezo huo hapa nchini.
Mshangama amesema, pia wadau wanatakiwa kuvisaidia vyama vya mikoa ili kuweza kukuza zaidi michezo na kupata vipaji vingi zaidi hapa nchini.





