Jumatano , 1st Jun , 2022

Mchezo wa fainali chini ya shirikisho la soka America ya kusini CONMEBOL na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA unao wakutanisha bingwa wa michuano ya Euro na bingwa wa Coppa America Italy dhidi ya Argentina utapigwa usiku wa leo Jumatano Juni 01.

Mchezo wa fainali ya 'CONMEBOL–UEFA Cup of Champions' Italia dhidi ya Argentina.

Mchezo huo wa kumsaka bingwa wa mabara unaojulikana kama 'CONMEBOL– UEFA Cup of Champions' mabingwa wa UEFA EURO 2020, Italia watachuana na mabingwa wa Copa America Argentina majira ya saa 3:45 usiku katika dimba la wembley jijini London nchini England.

Italia ilitinga fainali hiyo kwa kutwaa taji la Uropa msimu uliopita, baada ya kuwalaza Uingereza kwa mikwaju ya penalti katika fainali ya iliyopigwa katika dimba la Wembley na kutwaa taji lao la pili la bara la Ulaya.

Argentina nayo ilimaliza ukame baada ya kusubiri kwa miaka 28 kutwaa taji baada kuibukwa mabingwa wa Copa América 2021, kwa kuichapa Brazil bao 1-0 katika na kunyakua taji lao la 15 la michuano ya Copa América.

Mchezo huo wa fainali utachezwa mara moja kwa dakika 90 tu. Hakutakuwa na dakika 30 za muda wa ziada, hivyo kama dakika 90 zitamalizika kwa Sare basi wataenda moja kwa moja katika mikwaju ya Penati. Na Uteuzi wa waamuzi wanao chezesha mchezo huu, huchaguliwa kwa pamoja na mashirikisho hayo mawili CONMEBOL na UEFA.