Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao matatu (Hat-trick) kwenye ushindi huo na kumfanya afikishe mabao 10.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Chirwa akifunga bao la kwanza dakika ya 46 kabla ya kuongeza mengine katika dakika za 64 na 87.
Bao jingine la Yanga limefungwa na winga Emmanuel Martin hivyo kufanya Yanga ifikishe alama 34 na kupanda hadi nafasi ya pili ikiishusha Azam FC yenye alama 33 ambapo kesho itashuka dimbani kuivaa Simba.


