
CHANETA kimefurahishwa kwa kushuhudiwa timu za NIC ya Uganda, kwa upande wa Wanawake na Prisons ya Kenya upande wa wanaume, kuibuka mabingwa wa Michuano hiyo,
Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira amesema Mashindano hayo yalikuwa na Ushindani mkubwa kutokana na timu nyingi zilizoshiriki mashindano hayo kujiandaa vilivyo
Kibira amesema pamoja na changamoto kubwa yakukosa udhamini wa mashindano hayo, lakini wanawashukuru wadau wachache waliojitokeza na kutoa misaada mbalimbali na hatimaye mashindano hayo kufanyika kama yalivyopangwa.